Kanisa La Kristo Endamarariek, liko Ayaraati Karatu Arusha.
Kuhusu Kanisa
Kanisa la Kristo – Endamarariek ni kanisa linalojulikana kwa upendo wa kweli. Tunawakaribisha wageni kwa moyo mkunjufu, tunathamini kwa dhati huduma ya uinjilisti wa nyumba kwa nyumba, na pia tunashiriki kikamilifu katika mikutano ya uwanjani. Kupitia jitihada hizi, jamii inayotuzunguka imelifahamu vema kanisa hili, na watu wengi wameokolewa na kulipenda Kanisa la Kristo.rnrnKanisa hili limejengwa juu ya msingi wa upendo, ushirika wa dhati, na bidii katika kazi ya Bwana. Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2016, chini ya uongozi wa Mwalimu Martin na Mhubiri Mamiha, Kanisa la Kristo – Endamarariek limeendelea kukua na kustawi, na hadi sasa Wakristo zaidi ya 100 wamebatizwa, kwa utukufu wa Mungu. na kuanzishwa kwa Makanisa mapya mataturnrnKaribu sana! Ikiwa unatamani kufika au kushirikiana nasi katika kazi ya Bwana, tunakupokea kwa furaha. Njoo utembelee na tufanye kazi pamoja katika kusanyiko hili liliojaa upendo wa kweli na bidii ya kiroho.