Kichwa: KUSHUNDA HOFU
Andiko Kuu: Mathayo 6:25–34
Mwalimu: Momburi
Utangulizi
Kizazi chetu ni kizazi kilicho na maendeleo makubwa kuliko vyote vilivyopita kina utajiri, afya, elimu, na maendelea makubwa ya sayansi na Teknilojia.
Lakini jambo la kushangaza ndicho kizazi kilichosongwa zaidi na wasiwasi. Hata Wakristo hawako salama na tatizo hili. Wengine miguu yao haijasimama juu ya Mwamba wa Milele, macho yao hayajaelekezwa kwenye milima ambako msaada hutoka, wala mawazo yao hayajawekwa juu ya mambo ya mbinguni.
Yesu Kristo, katika Hotuba ya Mlimani, alizungumzia tatizo la Hofu moja kwa moja (Mathayo 6:25–34). Mafundisho yake yanaonyesha kwamba:
-Wasiwasi hauna maana,
-Wasiwasi haubadilishi chochote,
-Wasiwasi ni dalili ya imani ndogo,
-Wasiwasi ni ukosefu wa tumaini.
Lengo: Imani kwa Mungu hutufanya tushinde hofu ya maisha ya kila siku.
Vipengele vya Kujadili:
1. Ndege → Wasiwasi hauna maana (Mathayo 6:26)
Yesu alisema: “Tazameni ndege wa angani; hawapandi, wala hawavuni, wala hawana ghala, na Baba yenu wa mbinguni huwalisha. Je! Ninyi si bora kuliko hao?”
Ndege hawana wasiwasi juu ya kesho, lakini Mungu huwalisha.
Maombi kwa maisha yetu: Ikiwa Mungu anawajali viumbe vidogo, atatuzidishia zaidi sisi wana wake.
2. Mtu Mfupi → Wasiwasi haubadilishi chochote (Mathayo 6:27)
Yesu alisema: “Ni nani kati yenu kwa kujisumbua aweza kuongeza hata dhiraa moja katika kimo chake?”
Wasiwasi ni kama kuketi kwenye kiti cha mzunguko: unakupa shughuli, lakini haukufikishi popote.
Mwandishi mmoja alisema Hofu haijawahi:
Kulipa bili yoyote,
Kuendesha gari,
Kuandika wimbo,
Kufanya jambo la maana.
Maombi kwa maisha yetu: Wasiwasi hauongezi siku kwenye maisha yetu, bali unapunguza amani na furaha.
3. Maua → Wasiwasi ni dalili ya imani ndogo (Mathayo 6:28–30)
Yesu alisema: “Angalieni maua ya kondeni, jinsi yanavyokua; hayafanyi kazi wala hayasokoti. Lakini hata Sulemani katika fahari yake yote hakuvikwa kama moja la hayo.”
Mungu anayapamba maua yanayodumu siku chache tu. Je, hatatupamba sisi tulio wake milele?
Wasiwasi ni dalili ya imani ndogo.
Maombi kwa maisha yetu: Badala ya wasiwasi, tumwamini Mungu kwamba anatenda kwa faida yetu (tazama Warumi 8:28).
4. Mtoto → Wasiwasi ni ukosefu wa tumaini (Mathayo 6:32–33)
Watoto hawana wasiwasi juu ya chakula au nguo kwa sababu wanajua wazazi wao watawajali.
Tunapojisumbua ni kama kusema: “Siwezi kumwamini Baba yangu wa mbinguni.”
Yesu alisema: “Bali utafuteni kwanza ufalme wa Mungu na haki yake, na haya yote mtazidishiwa.” (Mathayo 6:33).
Maombi kwa maisha yetu: Tunapomweka Mungu kwanza, mambo mengine huanguka mahali pake.
Hitimisho
Yesu anatufundisha:
Ndege → Wasiwasi hauna maana.
Mtu mfupi → Wasiwasi haubadilishi chochote.
Maua → Wasiwasi ni dalili ya imani ndogo.
Mtoto → Wasiwasi ni ukosefu wa tumaini.
“Msijisumbue kwa ajili ya kesho; kwa maana kesho itajisumbua yenyewe” (Mathayo 6:34).
Wito:
Je, unajisumbua kuhusu kesho, afya, watoto, kazi au maisha yako ya kila siku?
Kumbuka: Mungu anakujali zaidi ya ndege, maua, na viumbe vyote.
Acha wasiwasi → Shika imani.
Acha hofu → Tafuta ufalme.
Acha kujisumbua → Mtwike Mungu mzigo wako (1 Petro 5:7).
Na kama Bado hauko NDANI ya Kristo ndio wakati sahihi WA kukata Shauri umwamini, umkiri , Utubu na Umvae Kwa njia ya Ubatizo upate Tumaini na uishinde hofu.📚🙏🏿